Home About Programs Impact Gallery Blog Contact Donate Now

DKT JAFO ATEMBELEA KATA YA KILUVYA AFIKA MPAKA DSJ

May 23, 2026
Kiluvya

About This Event

Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, Dkt. Selemani Jafo, Mei 2026 ametembelea taasisi mbalimbali za elimu zilizopo Kata ya Kiluvya, Wilaya ya Kisarawe, ikiwa ni sehemu ya kuendelea kuhamasisha maendeleo ya elimu na kusikiliza changamoto zinazowakabili wanafunzi pamoja na walimu.

Katika ziara hiyo, Dkt. Jafo alitembelea Shule ya Msingi Private, Shule ya Dimbeni pamoja na Chuo cha DSJ kinachojihusisha na mafunzo ya uandishi wa habari. Akiwa katika taasisi hizo, alipata fursa ya kuzungumza na wanafunzi, walimu pamoja na viongozi wa shule na chuo hicho kuhusu maendeleo ya elimu, mazingira ya kujifunzia na mahitaji muhimu ya miundombinu.

Akizungumza katika Chuo cha DSJ, Dkt. Jafo ameahidi kulipia ada za wanafunzi wawili wenye uhitaji maalum kupitia taasisi yake ya JAFO EDUCATION FOUNDATION, ikiwa ni sehemu ya mchango wake katika kuwawezesha vijana kupata elimu na kutimiza ndoto zao za kitaaluma.

Aidha, Mbunge huyo amepongeza uwekezaji mkubwa uliofanywa na uongozi wa chuo hicho katika Jimbo la Kisarawe, akieleza kuwa uwepo wa taasisi za elimu una mchango mkubwa katika kukuza taaluma, ajira na maendeleo ya vijana wa eneo hilo.

Sambamba na hilo, Dkt. Jafo ameahidi kuendelea kushirikiana na mamlaka husika kuhakikisha mazingira ya miundombinu, hususan barabara zinazoelekea kwenye taasisi hizo, yanaboreshwa ili kurahisisha huduma za elimu na usafiri kwa wanafunzi pamoja na wananchi wa maeneo hayo.

Comments (0)

Leave a Comment

No comments yet. Be the first to comment!